KMC YAZIPIGIA HESABU POINTI ZA GEITA GOLD

CHRISTINA Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa kwa sasa wanafanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Geita Gold unaotarajiwa kuchezwa Aprili 23,Uwanja wa Nyankumbu.

 Mwagala amesema kuwa mchezo wao uliopita walipata pointi hivyo hesabu zao ni kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Geita Gold.

“Tulicheza usiku mbele ya Kagera Sugar na tulipata pointi moja ambayo ni kubwa kwetu tunawapongeza wachezaji wetu kwa kuwa kawaida yao ni kucheza mpira unaoeleweka na burudani.

“Ilikuwa ni kwa mara ya kwanza saa 3 usiku tukiwa ugenini hawa ni wanaume wa shoka na wapo tayari kuipambania timu.

“Pamoja na kwamba tumepata pointi moja sasa tunakwenda kusaka pointi tatu za Geita Gold ili kuweza kurudi na zawadi nzuri ya Pasaka kwa mashabiki wetu wa Dar,” amesema Mwagala.

Kwenye msimamo KMC ipo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 20 itakutana na Geita Gold iliyo nafasi ya 9 na pointi 24.