SIMBA KUTINGA CAF KISA KOCHA ORLANDO PIRATES

BREAKING:Klabu ya Simba leo Aprili 19 imetoa taarifa ya kuhusu malalamiko ya uongo ya Kocha Mkuu wa Orlando Pirates, Mandla Nickazi alizotoa baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Orlando Pirates ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba Simba imechukizwa na maneno ya kashfa yaliyotolewa na kocha huyo ambayo yanatabaisha ukosefu wa taaluma na ukiukwaji wa maadili kwa taaluma ya kocha.

Maneno hayo yanakiuka ule ukweli ambao Simba wamekuwa wakiuheshimu kwa kutoa huduma bora kwa wageni wote wanaokuja Tanzania.

Simba wameeleza kuwa waliaandaa huduma za usafiri ikiwa ni pamoja na basi kubwa pamoja na gari dogo lakini wapinzani wao walikataa.

Pia waliwashauri kukaa hotel ya karibu na uwanja lakini walishindwa kukaa na kuchagua kukaa nje kidogo ya mji hali iliyopelekea waweze kuchelewa mazoezini kwa zaidi ya saa moja.

Imeongeza kuwa Orlando Pirates waligoma kutumia mlango wa kawaida na badala yake walipita kwenye mlango wa kuingilia kwa chumba cha Wanahabari.

Kufuatia kwa kauli hizo Simba imeweka wazi kuwa itawasilisha malalamiko rasmi Shirikisho a Soka Afrika,(CAF) na kupitia balozi zote za nchi mbili kueleza yote yaliyoelekezwa na kocha huyo.

Kocha huyo baada ya mchezo kuisha alisema kuwa Simba walipendelewa na VAR haikuweza kutumika kwenye mchezo huo ambapo bao la penalti halikuwa halali.