KLABU ya Njombe Mji leo Aprili 19 imepoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Rhino Rangers katika mchezo wa 8 bora.
Mtupiaji Ibrahim Mdaki alitumia mtindo wa kupekecha kama Pape Sakho wa Simba kushangilia na kuimaliza mazima Njombe Mji.
Katika mchezo mwingine wa kundi A ilishuhudiwa Alliance FC wakitoshana nguvu na Tunduru Korosho.
Baada ya dk 90 ubao ulisoma Alliance 2-2 Tunduru Korosho na kuwafanya kugawana pointi mojamoja.
Watupiaji kwa Tunduru Korosho ni Kassimu Kilungo na Amos Mataji huku kwa Alliance mtupiaji akiwa ni Abdul Migomba.