KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu,Nasreddine Nabi mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Mara ya mwisho Yanga kucheza Uwanja wa Lake Tanganyika ilikuwa ni Julai 25,2021 ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Simba,FA.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga,Hassan Bumbuli amesema kuwa wamepata barua kuhusu Ruvu Shooting kupeleka Uwanja wa Lake Tanganyika mchezo wao.
“Tumepata barua kwamba jamaa wamepeleka mechi yao Kigoma,tunawaambia wanachama na mashabiki wasiwe na wasiwasi kwa sababu ipo kwenye kanuni,tutakwenda kucheza hiyo mechi Yanga kila uwanja ni nyumbani,”.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Mei 4,2022 ukiwa ni wa mzunguko wa pili.