KANOUNTE,ONYANGO KUIKOSA ORLANDO PIRATES KWA MKAPA

KIUNGO wa kazi ngumu ndani ya Simba, Sadio Kanoute kesho Aprili 17 anatarajiwa kuwakosa wapinzani wao Orlando Pirates kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya kwanza Kombe la Shirikisho.

Sababu kubwa ya kiungo huyo mwenye bao moja kwenye hatua za makundi kuwakosa wapinzani hao ni mkusanyiko wa kadi tatu za njano ambazo alipata kwenye mechi za kimataifa.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco ina kiarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo huo ambapo wataanza kete ya kwanza nyumbani kisha watakwenda ugenini kumaliza kete ya pili.

Mbali na Kanoute pia Joash Onyango naye anatarajiwa kuukosa mchezo huo mgumu kwa Simba.

Kwa mujibu wa Franco amesema wapo tayari kwa mchezo huo na watapambana kupata ushindi.

“Tunahitaji kupata ushindi kwenye mchezo wetu na tunatambua kwamba takuwa mgumu ila tutafanya vizuri, kila mmoja anajua umuhimu wa mchezo wetu huo,”.