YANGA V GEITA GOLD,NGOMA ILIPIGWA HIVI,NABI MAJANGA

KAZI ilikuwa kubwa kwenye msako wa ushindi Uwanja wa Mkapa kati ya Yanga dhidi ya Geita mwisho wa siku bahati ikawa kwa upande wa Yanga.

Geita Gold waliweza kuonyesha burudani makini ila mwisho wakapoteza kwa penalti 7-6 dk 90 zilikamilika kwa kufungana bao 1-1 ilikuwa namna hii msako wa kutinga nusu fainali:-

Yaliyolenga lango

Kwa Yanga Dickson Job alipiga shuti dk ya 1 lililenga lango kiungo Zawad Mauya aliweza kupiga shuti moja lililolenga lango ilikuwa dk ya 38  na George Mpole kwa Geita Gold alipiga dk ya 58.

Kazi ya mapigo huru

Ni Said Ntibanzokiza kwa Yanga alipewa jukumu la kupiga kona kwenye mchezo wa juzi ambapo alipiga kona 10 ilikuwa dk ya 6,34,37,38,47,48,49,51,77,77.

Kwa Geita Gold Amos Kadikilo alipiga kona dk ya14,20 na 46.

Walibadili mambo

Ni bao la Hoffem Chikola dk ya 88 liliweza kuwapa matumaini Geita Gold kuweza kutinga hatua ya nusu fainali ambapo nyota huyo aliweza kupachika bao hilo akitokea benchi alipokuwa akisoma mchezo.

Katika dk za lala salama beki Geita Gold alijichanganya kwenye kuokoa mpira ukagusa mkono ndani ya 18 ikafunikwa penalti ambayo ilijazwa kimiani na Djuma Shabadn dk 90+4.

Waliokosa penalti

Baada ya kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 ikabidi mshindi asakwe kwa changamoto ya penalti na Yanga iliweza kushinda 7-6 za Geita Gold.

Kwa Yanga ni Diarra Djigui yeye alikosa penalti yake.

Kwa upande wa Geita Gold ni Maka Edward pamoja na Juma Mahadhi penalti za hawa ziliokolewa na kipa Diarra ambaye alikuwa ni shujaa wa mchezo.

Hawa walifunga

Sebusebu Samson alikuwa langoni kwa Geita Gold alionja joto ya penalti za Yanick Bangala,Jesus Moloko,Said Ntibanzokiza,Fiston Mayele,Djuma Shaban,Bakari Mwamnyeto na Dickson Job.

Diarra alikutana na michomo ya David Kameta ,George Mpole,Yusuph Kagoma,Adeyum Saleh,Chikola na Kelvin Yondan.

Majanga

Nabi alipata majanga baada ya kuweza kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi kutokana na kile alichoonekana kujibizana na mwamuzi wa akiba baada ya mchezo kukamilika.

Kwa maana hiyo, Nabi ataukosa mchezo wa Kariakoo Dabi kati ya Yanga  v Simba utakochezwa Uwanja wa Mkapa.

Maneno ya makocha

Cedrick Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wengi walikuwa wametumia nguvu kubwa mbele ya Azam FC hivyo walikuwa wakipambana.

“Tumetoka kucheza mchezo mgumu dhidi ya Azam FC na wachezaji walitumia nguvu kubwa kuweza kushinda na hapa mbele ya Geita Gold ambacho tulikuwa tunahitaji ni ushindi.

“Mechi za mtoano huwa zinakuwa hazina muda wa kuweza urudia hivyo ambacho tumekipata tunasema tumestahili na tulipata upinzani mkubwa kutoka kwa Geita Gold.

Fred Felix Minziro, Kocha Mkuu wa Geita Gold amesema kuwa hakukuwa na namna ambayo wangefanya hasa kwenye penalti.

“Kwa kucheza vijana wamecheza na tazama namna walivyoweza kupata bao kisha nasi tukafungwa, kwa kutolewa kwa changamoto ya penalti hakuna ambaye ninaweza kumlaumu,” .

Uso kwa uso na Simba/Pamba

Kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali sasa ni uso kwa uso na mshindi wa mchezo kati ya Simba v Pamba FC ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa na utapangiwa tarehe.

@Dizo_Click.