SIMBA WATAJA SABABU YA KUSHINDWA KUPATA MATOKEO

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kuna ugumu mkubwa wa kupata matokeo kutokana na ubora wa viwanja pamoja na kushindwa kutumia nafasi ambazo wanazipata.

Mechi mbili ugenini, Pablo kaambulia pointi nne huku akipoteza pointi mbili kwenye msako wa pointi sita, mchezo wake ujao ni dhidi ya Orlando Pirates ambao wa ni wa Kombe la Shirikisho.

Mbele ya Coastal Union alishinda kwa mabao 2-1 kisha ule dhidi ya Polisi Tanzania waligawana pointi mojamoja kwa sare ya bila kufungana.

Pablo amesema:”Ninaweza nikasema kwamba kila mchezo ambao tunacheza ni mgumu huku tukitengeneza nafasi na kushindwa kuzitumia hilo ni letu na tutafanyia kazi ili kuwa bora kwa mechi zijazo.

“Kuhusu viwanja kwa kweli hilo liache maana linaonekana na inajulikana pale ambapo tunacheza, muhimu kwetu ni kuona tunapata matokeo hakuna kingine ambacho tunahitaji,”.

Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 41 baada ya kucheza mechi 19 huku Polisi Tanzania ikiwa na pointi 24 nafasi ya 8.