SIMBA HESABU ZAO KIMATAIFA ZIPO HIVI

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kwa sasa akili zao ni kuelekea mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Orlando Pirates.

Aprili 17,2022 Simba itakuwa na mchezo wa kusaka ushindi dhidi ya Orlando Pirates Uwanja wa Mkapa unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari,Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa tayari wameanza kuuza tiketi na maandalizi yanaendelea.

“Kama kawaida yetu maandalizi kuelekea mchezo wetu yanaendelea na kesho tutakuwa katika tawi la Temeke katika tawi la tunawakera kwa ajili ya kutoa hamasa kwa mashabiki kuweza kujitokeza uwanjani.

“Tumeruhusiwa mashabiki 60,000 hii ina maana kwamba kila mmoja ambaye atakuwa nyumbani ajitokeze uwanjani na tiketi anunue mapema kwa ajili ya kuepuka usumbufu.

“Kikubwa tunahitaji ushindi kwenye mchezo wetu ili kusonga mbele hatua ya nusu fainali kisha fainali,” amesema.