YANGA YAPANIA KUSEPA NA UBINGWA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa mpango kazi wao namba moja ni kuweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ulio mikononi mwa Simba.

Kwenye msimamo, Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi ni namba moja ikiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 19 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa wanatambua kwamba ushindani ni mkubwa lakini wanahitaji kutwaa ubingwa.

“Kila siku tunafanya tathmini ya kile ambacho tunakihitaji na kipaumbele chetu ni kuweza kuona kwamba tunatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara inawezekana na kila mchezaji anajua.

“Ambacho tunakifanya ni kusaka ushindi kila mechi kwa umuhimu mkubwa,mashabiki wamekuwa pamoja nasi na tunaomba wazidi kuendelea kuwa pamoja nasi kwa kuwa wanaongeza ile hamasa kwa wachezaji katika kutafuta ushindi,”.

Kinara wa utupiaji ni Fiston Mayele ambaye ametupia mabao 11 kibindoni na alikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Januari 2022 Aprili 6, Uwanja wa Azam Complex.