NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa anahitaji kushinda kwenye mechi zake zote ikiwa ni pamoja na dabi mbili mbele ya Azam FC na Simba.
Aprili 6, Yanga itamenyana na Azam FC Uwanja wa Azam Complex kisha itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Simba Aprili 30.
Akizungumza na Spoti Xtra,Nabi alisema kuwa ni mechi ngumu ambazo zipo mbele yake ikiwa ni pamoja na dabu ila ambacho anahitaji ni ushindi.
“Unaona kwamba ratiba inatuhitaji tuweze kucheza na tuna mchezo dhidi ya Azam FC na tukimaliza mchezo huo tutakuwa na kazi dhidi ya Simba.
“Sio kazi nyepesi kwetu kutokana na kila timu kuhitaji kushinda pale ambapo tutakutana,Imani yetu ni kuona tunashinda hasa mechi hizi za dabi,” alisema Nabi.
Kwenye msimamo Yanga ni vinara wakiwa na pointi 48 baada ya kucheza mechi 18.