NNAUYE:USHINDI WA SIMBA NI MUHIMU KWA NCHI

NAPE Nnauye,Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema kuwa ushindi wa leo kwa Simba ni muhimu kwa nchi.

Simba ina kibarua cha kusaka pointi tatu muhimu mbele ya USGN mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ni hatua ya makundi.

Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa leo unaotarajiwa kuchezwa saa 4:00 usiku.

Kiongozi huyo amesema:”Ushindi wa Simba leo ni muhimu kwa nchi yetu nina imani kwamba Simba watapata matokeo hivyo bila kujali ushabiki tujitokeze kuishangilia Simba.

“Niwatie moyo wawakilishi wetu kuhusu mchezo wa leo na Serikali imejipanga vizuri katika mambo ya usalama,tutakwenda salama na tutarudi salama,”.

Simba inasaka tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali na ili iweze kufikia hatua hiyo lazima ishinde mchezo wa leo dhidi ya USGN.