YANGA YAREJESHA SHUKRAN KWA JAMII

WACHEZAJI wa Yanga pamoja na benchi la ufundi leo Aprili Mosi wamepata muda wa kuweza kutoa misaada kwa vituo mbalimbali vya Watoto Yatima.

Hii ni maalumu kwa ajili ya kuelekea mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Ni Kampuni ya GSM kwa kushirikiana na Yanga weweza kuyafanya hayo ikiwa ni kurejesha shukrani kwa jamii.

Mbali na kutoa msaada pia Watoto walipata muda wa kuweza kucheza pamoja na wachezaji na viongozi wa Yanga.

Shughuli nzima imefanyika kwenye Viwanja vya Gymkhana,Dar.