ADEBAYO AWEKA WAZI NAMNA ATAKAVYOIMALIZA SIMBA

KIUNGO mshambuliaji wa US Gendarmerie, Victorien Adebayor, ameweka wazi kuwa atahakikisha anapambana kwa nguvu ili kuisaidia timu yake kupata ushindi dhidi ya Simba,Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mchezo huo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho utapigwa Jumapili ya Aprili 3, unatarajia kuwa mkali kwani kila timu ina nafasi ya kwenda robo fainali ikiwa itashinda mchezo huo, wageni wanatarajia kutua nchini kesho Alhamisi.

Licha ya hivyo, Adebayor ambaye amefunga mabao matatu kwenye michuano hiyo anahusishwa kutakiwa na Simba na hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Try Again aliweka wazi kuwa wangependa kumsajili nyota huyo.

 Adebayor amesema kuwa. “Licha ya mchezo huu na Simba kuwa muhimu sana kwetu na kwao ila nitakuwa na furaha sana kuwaona mashabiki wa Simba na kuweza kucheza nao nyumbani.

“Kwa upande wangu maandalizi ya mchezo huo yapo vizuri na sina presha yoyote kuelekea mchezo huo na nitajitahidi kufanya vizuri ili kuisaidia timu yangu.”