YANGA YASHINDA 3-2 MAFUNZO FC,BALAMA ATUPIA

MECHI ya kirafiki imekamilika Uwanja wa Azam Complex leo Machi 30 ambapo Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mafunzo FC.

Mabao yamefungwa na Mapinduzi Balama dk ya 19 Heritier Makambo dk ya 52 na lile la ushindi limefungwa na Fiston Mayele dk ya 71 kwa mkwaju wa penalti ilikuwa ni kwa upande wa Yanga.

Kwa upande wa Mafunzo FC ambao walianza kwa kasi kwenye mchezo wa leo ni mabao ya Ahmed dk ya 9 na Abdulhakim dk ya 55 yaliwezwa kujazwa kimiani.

Mafunzo FC walianza kupata bao la kuongoza Yanga wakamaliza kazi kwa kupata bao la ushindi kipindi cha pili.

Mapinduzi ameweza kupachika bao hilo baada ya kuwa nje kwa muda akitibu majeraha hivyo ni mwanzo mzuri kwa mzawa huyo kuweza kurejea uwanjani.

Pia mchezo wa leo ni maalumu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya Azam FC ambao utakuwa ni wa Ligi Kuu na unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.