YANGA YATENGA DAKIKA 90 ZA KUANDAA KIKOSI KAZI

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa utatumia dk 90 kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Mafunzo kwa ajili ya kuandaa kikosi kazi kitakachomenyana na Azam FC.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi imekusanya pointi 48 ikiwa nafasi ya kwanza inatarajiwa kumenyana na Azam FC iliyo nafasi ya 3 na pointi 28 zote zimecheza mechi 18.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 6,Uwanja wa Azam Complex.

“Tunacheza na Mafunzo ya Zanzibar kwenye mechi ya kirafiki ni maandalizi kuelekea mechi zetu za Aprili hususani ya Aprili 6 dhidi ya Azam FC.

“Hiki ni kipimo kizuri kwa kocha ili kuweza kujua changamoto za wachezaji na kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa kuikabili Azam FC ambayo ni muhimu kwetu,” amesema Manara.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza Azam FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo Machi 30 na Aza, FC wao walicheza jana Machi 29 dhidi ya DTB inayoshiriki Championship.