PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa wanahitaji ushindi katika mchezo wao wa Jumapili dhidi ya US Gendarmerie unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Simba iliyo nafasi ya tatu ina kazi ya kusaka pointi tatu muhimu ili kuweza kukata tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali.
Tayari kikosi kipo kambini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao utakuwa na mashabiki 35,000 walioruhusiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Pablo amesema:”Tunajua tunahitaji kushinda katika mchezo wetu ili kuwa furaha mashabiki wetu,naamini watajitokeza kwa wingi Jumapili,”.
Ni Hassan Dilunga anatarajiwa kuukosa mchezo huo kwa kuwa bado hajawa fiti na katika mazoezi ya jana Machi 28 alipata maumivu inategemea namna atakavyokuwa.