HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zote za kwenye ligi ikiwa ni pamoja na mchezo wao dhidi ya Azam FC.
Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 48 baada ya kucheza mechi 18 inatarajiwa kukutana na Azam FC Aprili 6, Uwanja wa Azam Complex.
Manara amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu lakini wanaamini kwamba watapata ushindi kwenye mchezo huo.
“Tunatambua kwamba mchezo wetu utakuwa mgumu lakini tupo tayari kwa ajili ya kusaka ushindi na tuna amini kwamba nawezekana mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema
Machi 30 Yanga inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mafunzo Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.
Tayari wachezaji wameanza mazoezi na miongoni mwao ni pamoja na kiungo Dennis Nkane, Fiston Mayele na Yassin Mstafa.