CHELSEA YAPIGA 9-0 LEICESTER

TIMU ya Wanawake ya Chelsea imeibuka na ushindi wa mabao 9-0 dhidi ya timu ya Wanawake ya Leicester City.

Mchezo huo wa Ligi ya Wanawake ulichezwa Uwanja wa The King Power Jumapili ya Machi 27,2022.

Mabao ya Guro Reiten ambaye alitupia mabao mawili ilikuwa dk ya 3 na 45+5 huku Sam Kerr yeye alitupia mawili dk 3 ma 47, Beth England naye alitupia mbili dk 7,28.

Aniek Nouwen alitupia dk 11, Lauren James alitupia dk 88 na msumari wa 9 ulipachikwa dk ya 90 na Jessie Fleming.