KAMPUNI ya Mawasiliano Tanzania ya Halotel Tanzania,leo Machi 28 imezindua promosheni ya ‘Shinda na Halopesa’ itakayotoa fursa kwa wateja kuweza kushinda fedha taslimu pamoja na Pikipiki maarufu kama ‘Bodaboda’ mpya kabisa.
Promosheni hii itadumu kwa muda wa wiki 8 ni maalumu kwa wateja wa HaloPesa na ni jumla ya wateja 72 watashinda zawadi mbalimbali zitakazotolewa katika kipindi hicho.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa HaloPesa,Magesa Wandwi amesema kuwa fursa hii ni kwa wateja wa HaloPesa ambao watakuwa wakifanya miamala kwa kutumia huduma ya HaloPesa kila siku.
“Promosheni ya Shinda na HaloPesa ni ya muda wa wiki 8 ambayo itakuwa na zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha kuanzia shilingi elfu hamsini,(50,000) na laki moja,(100,000) kila siku na wateja 8 watajishindia Pilipiki,(Bodaboda) mpya kabisa.
“Washindi hao watapatikana kupitia miamala ambayo wanaifanya iwe ni kutuma pesa kutoka HaloPesa kwenda HaloPesa,HaloPesa kwenda mitandao mingine,HaloPesa kwenda benki iwe ni kwa kununua muda wa maongezi na kulipa vifurushi hiyo yote itawafanya waweze kujishindia zawadi.
“Wanachotakiwa kufanya ni kufanya miamala mingi kadri wawezavyo ili waweze kupata zawadi zao na tuna mawakala wengi Tanzania ambao wanatoa huduma zetu” amesema Magesa.