KIUNGO wa Yanga, Jesus Moloko, amefunguka kuwa kwa sasa anatamani sana kurejea kwenye kikosi hicho ili kuendeleza mapambano ya kulisaka taji la ligi kuu msimu huu.
Moloko ambaye ameanza mazoezi na timu hiyo, anadai kuwa alikuwa anajisikia vibaya kuwa nje ya timu kwa sababu ya majeraha kwa kuwa mara zote amekuwa na kiu ya kutaka kuipigania timu hiyo.
Moloko amesema sasa anajisikia vizuri kuanza mazoezi na timu hiyo ambayo kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam FC ambao utapigwa Aprili 6, mwaka huu.
“Nimerudi mazoezini sasa na timu yangu na tunafanya maandalizi pamoja ya kujiandaa na mchezo wetu na Azam FC. Sikuwa na furaha sana kuwa nje ya uwanja kwa muda wote.
“Sasa nimerudi kuipambania timu yangu, kwa sababu wote tunalitaka taji la ligi kuu msimu huu,” amesema Moloko.