WALIOPEWA NAFASI TAIFA STARS WAFANYE KWELI

MAZINGIRA ambayo yapo kwa sasa kwa wachezaji walioitwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni rafiki kwao kufanya kazi kwelikweli ili kuweza kupata ushindi.

Hizi mechi ambazo zipo kwenye kalenda ya FIFA ni muhimu kwa wachezaji kuzipa uzito mkubwa na kufanya vizuri ili kupata matokeo.

Ukiangalia namna ambavyo wachezaji wanapata nafasi kikosi cha kwanza na kuonyesha uwezo hilo ni jambo ambalo linapaswa kuwa endelevu.

Wapo ambao wanashindwa kuonyesha makeke yao yote hii ni nafasi ambayo haipaswi kubezwa hata kidogo hivyo wale ambao wanachezea nafasi hizi watakuja kuzikumbuka.

Pongezi kwa kila mchezaji ambaye aliweza kucheza kwenye ule mchezo wa kwanza dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kila mmoja alionekana akifanya vizuri na kupata matokeo.

Makosa yapo hilo huwezi kuficha hasa kwenye upande wa ulinzi kama ambavyo mwalimu alisema hapo ni muhimu kuweza kufanyia kazi kwa mechi zijazo.

Pia kwenye upande wa ushambuliaji bado ni tatizo ambalo linahitaji tisa hasa kwa mechi zijazo kwani kinachokosekana ni umaliziaji kwenye mechi ambazo tunacheza.

Pongezi kwa mashabiki ambao wamekuwa wakijitokeza kwenye mechi hizi nina amini kwamba wanakipata kile ambacho wanastahili na wachezaji kazi yenu iwe kusaka ushindi bila kuogopa.