MABOSI WAJITOKEZA KUINUNUA CHELSEA

IMERIPOTIWA kuwa familia ya Ricketts ipo kwenye orodha ya wale ambao wanahitaji kuinunua Klabu ya Chelsea inayomiliki Uwanja wa Stamford Bridge.

Pia wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa zamani wa Liverpool Martin Broughton.

Kwa mara ya kwanza ililipotiwa na Sky News siku ya Alhamisi huku Boston Celtics na mmiliki wa kampuni ya Atalanta Stephen Pagliuca naye akiwa katika orodha hiyo.

Watu wanaoisapoti Chelsea wameweka bayana kuwa wana imani na familia ya Ricketts katika suala la kuweza kuiendesha timu hiyo.