TIMI ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars leo Machi 23 imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mchezo wa kirafiki ambao upo kwenye kalenda ya FIFA.
Ni bao la Novatus Dismas dk 9 aliweza kupachika bao hilo kwa pigo huru akiwa nje ya 18 baada ya kiungo Feisal Salum kuchezewa faulo na kipa akafanya makosa katika kuokoa.
Bao la pili lilipachikwa na mshambuliaji Mbwana Samata ilikiwa dk 61 kwa pasi ya Farid Mussa ambaye aliingia kipindi cha pili.
George Mpole akitokea benchi naye pia alipachika bao la tatu dk 90.
Lile la Jamhuri ya kati ni Yawanendji Theodore dk 65 kwa mkwaju wa penalti.
Pia mchezaji Toropite Tresor alionyeshwa nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano na kufanya Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kukamilisha dk 90 ikiwa pungufu.