MASHINDANO YA GOFI EUROPE TOUR KUFANYIKA KILIMANJARO

SERIKALI kwa kushirikiana na Chama cha mchezo wa Gofu Tanzania (TGU), kimethibitisha kuwa wenyeji wa mashindano ya Gofu Europe Tour yatakayofanyika Aprili 7 hadi 10 mwaka huu katika viwanja vya Kilimanjaro Jijini Arusha.

Mashindano hayo yana lengo la kuunga mkono wa juhudi ya serikali chini ya Rais, Samia Suluhu Hassan kuendeleza utalii nchini.

 Mwenyekiti wa TGU, Chris Martin amesema ni mara ya kwanza Tanzania kuandaa mashindano hayo makubwa ambayo yatashirikisha mataifa mbalimbali.

Amesema wachezaji 156 wamethibitisha kushiriki mashindano hayo ambapo Tanzania imetoa wachezaji 12, Kenya, Uganda, Rwanda na Malawi kumetoa wachezaji wawili.

“Hapa nchini tutakuwa na wawakilishi 12 kutoka katika klabu tofauti, watakuwepo wachezaji wengine kutoka bara la Ulaya, Asia na mataifa mengine nina imani mashindano haya yatatoa fursa kwa kutangaza utalii wa Tanzani,” alisema Martin.

Amesema TGU imeomba Tanzania kuandaa mashindano haya ambayo mwaka jana yalifanyika nchini Kenya yanatarajia tena kufanyika mwakani kwa mara ya pili kuwa wenyeji.

“Tunaendeleza kampeni ya Royal Tour ambayo Rais wetu Mama Samia ameianzisha kwa ajili ya kutangaza Utalii wa ndani na vitu vinavyopatikana hapa nchini,” alisema Martin.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Maendeleo ya Michezo nchini, Yusuph Singo amesema ni jambo nzuri kuona mashindano hayo yanatangaza utalii wa taifa, lakini serikali itakutana na Chama cha TGU kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya mashindano hayo.

“Kwa sasa hatuwezi kuzungumza lolote kwa sababu serikali tuna mpango wa kukutana na uongozi wa Chama cha gofu kwa ajili ya maandalizi ya mashindano baada ya hapo tutatoa tamko kuhusu uwenyeji wa mashindano hayo,” amesema Singo.

Katibu wa maandalizi ya mashindano hayo, Enock Magile amesema sifa za wachezaji ambao watashiriki lazima wawe na kiwango kizuri katika rekodi ya mchezo huo.

Amesema watacheza ambao watakuwa na viwango hivyo watapita bila tatizo lolote lile kwa ajili ya kuitangaza taifa na kuonyesha uwezo wao.