FISTON MAYELE ATAJA SABABU ZA KUFUNGA MABAO 10

FISTON Mayele mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kuweza kufunga mabao 10 ndani ya ligi ni kutimiza majukumu yake pamoja na kufanya kile anachokifanya mazoezini.

Msimu wa 2021/22 Mayele amecheza mechi 18 na kufunga mabao 10 kati ya 31 ambayo yamefungwa na timu hiyo na ametoa pasi 3 za mabao.

Mayele amesema kuwa anafunga kila anapopata nafasi ya kufunga kwa kuwa ni kazi yake kila anapokuwa uwanjani.

“Ninafunga kwa sababu ni majukumu yangu pia  ninajua kwamba ili timu iweze kushinda inahitaji kuweza kufunga jambo ambalo linafanya ninakuwa bora.

“Kitu kingine ni kwamba mazoezi ambayo ninafanya ni kitu muhimu pia kwa kuwa yananifanya ninakuwa imara na ninapenda kuona inakuwa hivyo kila mechi,” amesema Mayele.