YANGA WAWAPOTEZA MABINGWA WATETEZI KWA POINTI KIBAO

YANGA imewaacha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba kwa tofauti ya pointi 11 kibindoni.

Yanga ina pointi 48 baada ya kucheza mechi 18 na Simba ina pointi 37 baada ya kucheza mechi 17.

Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC uliochezwa jana Uwanja wa Mkapa kumewapa nguvu vinara hao kujikita zaidi hapo.

Simba wao wana mchezo mmoja mkononi kwa kuwa wanaiwakilisha nchi kimataifa katika Kombe la Shirikisho na hata wakishinda bado watakuwa wameachwa kwa pointi 8.