WAWILI WASHINDA MAMILIONI YA BETBONANZA

JUMLA ya washindi Wawili kutoka Vodacom na Airtel leo Jumanne asubuhi wameibuka washindi wa vitita vya Shilingi Milioni Moja kila mmoja katika droo ya kwanza ya wiki ya Bet Bonanza ya Sportpesa huku akiwataja washindi hao ni Seif Ramdshani wa Shinyanga na Nyange kutoka Tabata.

Droo hiyo ni sehemu ya promosheni ya Bet Bonanza ya Sportpesa na pia ni muendelezo wa zawadi ambazo zinatolewa katika kipindi hiki ambacho ligi mbali zinazochezwa kwa ushirikiano na kampuni za simu Vodacom, Airtel na Halotel.

Akizungumza baada ya droo iliyochezeshwa Makao Makuu ya Sportpesa, Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa Sportpesa Sabrina Msuya alianza kuwapongeza washindi hao kwa kuibuka washindi wa wiki ya kwanza ya promosheni.

“Kwa hakika Watanzania hawa wawili wamejishindia vitita hivi vya shilingi Milioni Moja na hivyo kuwataka wateja wenzao ambao wanatumia huduma za makampuni haya kuendelea kucheza mara nyingi kadri iwezekanavyo ili na wao washinde zawadi hizi.

‘’Nawasisitiza Watanzania hasa wateja wa Vodacom, Airtel na Halotel kuchukua fursa hii ya promosheni hii ya Bet Bonanza kwani kuna zawadi ya Shilingi 20, 000 kila siku, zawadi ya Shilingi Milioni Moja kwa washindi watatu kama hii kila wiki na zawadi kubwa kabisa ya Shilingi 15,888,000 siku ya kufunga promosheni,’’amesema Sabrina.

Ikumbukwe promosheni hii ilizinduliwa rasmi siku ya Machi 8, mwaka huu ambayo inajumuisha zawadi za Shilingi 20, 000 kila siku, zawadi za Milioni Moja kwa washindi watatu kila wiki, na zawadi ya Shilingi 15,888,000 siku ya kufunga kampeni.

Ili kujisajili na kucheza na Sportpesa Piga *150*87# au tembelea www.sportesa.co.tz au download APP yetu.