WAPINZANI wa Simba kimataifa RS Berkane ya Morocco walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kuikabili Simba Uwanja wa Mkapa na miongoni mwa nyota ambao walikuwepo ni pamoja na Fiston Abdulazack na Tuisila Kisinda ambao waliwahi kucheza Klabu ya Yanga.
Mchezo wa kwanza wa kundi uliochezwa nchini Morocco, Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 hivyo leo unatarajiwa kuwa mchezo wa kisasi kwa Simba ambao wameweka wazi kwamba wanahitaji ushindi kama ambavyo Berkane wanahitaji.