MCHEZO WA HISANI YANGA WATOSHANA NGUVU NA WASOMALI

KWENYE mchezo wa Hisani uliochezwa Uwanja wa Azam Complex kati ya Yanga dhidi ya timu ya taifa ya Somalia timu hizo mbili zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Bao la Somalia lilifungwa na Zakaria na bao la Yanga lilifungwa na kiungo Chico Ushindi ambaye alifunga bao hilo akitumia krosi ya Djuma Shaban.

Mchezo huo ulihudhuriwa na mashabiki wengi waliojitokeza kwa wingi huku Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara akiwashukuru mashabiki pamoja na wote waliojitoa kwa ajili ya mchezo huo pamoja na michango yao.

Pia Ali Kimara na Wazazi wake walipata nafasi ya kuwasalimia wanachama na mashabiki wa Yanga kwenye mchezo huo maalum wa kirafiki wa kuchangia Taasisi ya Ali Kimara.