YANGA KUCHEZA MCHEZO WA HISANI KESHO AZAM COMPLEX

KLABU ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunissia kesho, Jumamosi Machi 12 inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Somalia.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa  Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya KMC.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema:”Yanga tutacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Somalia Jumamosi Machi 12, 2022 saa 1:00 Usiku kwenye uwanja wa Azam Complex.

“Lengo ni kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia Taasisi ya Ali Kimara ( Ali Kimara Rare Disease Foundation). Utakuwa ni mchezo mgumu lakini utakuwa pia sehemu ya maandalizi kuelekea kwenye mechi zetu za ligii,”.

Yanga imekuwa na mtindo wa kurejesha hisani kwa jamii ambapo kwa sasa mchezo huo pia utakuwa ni wa hisani.