MTAMBO WA MABAO YANGA UPO KAMILI GADO

FISTON Mayele, nyota wa kikosi cha Yanga yupo kamili gado kwa ajili ya mwendelezo wa mechi za ushindani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Mayele alipata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Kwenye mchezo huo Mayele alikwama kuyeyusha dakika 90 na aliweza kutoka dakika ya 70 nafasi yake ikachukuliwa na nyota mwingine Heritier Makambo.

Kibindoni Mayele ametupia mabao 10 na ana pasi tatu za mabao kwenye mechi 17 ambazo amecheza kwa msimu wa 2021/22 ikiwa ni msimu wake wa kwanza kwenye ligi.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa hali ya wachezaji wote ipo salama na kila mchezaji yupo sawa.

“Kuhusu maendeleo ya kikosi chetu ambacho ni namba moja kikiwa juu kwa alama 8 za yule aliyepo nyuma, wachezaji wameanza mazoezi na tutarejea Avic Town kwa ajili ya maandalizi yetu.

“Majeruhi wameanza kurejea kikosini, Kibwana Shomari, Ninja, Aucho,utaona sasa ile Ambulace inaanza kuachana na wachezaji wetu hii ni habari njema kwa timu, klabu.

“Pale unapokuwa na majeruhi unakuwa na changamoto kwa mwalimu, Fiston Mayele yupo tayari na ameanza mazoezi, kipenzi chenu mzee wa kugudema yupo tayari kwa ajili mchezo ujao,”.