SIMBA:RS BERKANE WAMEKUJA WAKATI MBAYA,MUGALU AREJEA

AHMED Ally Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa wapinzani wao wamewakuta wakiwa kamili kutokana na wachezaji wote kuwa tayari kwa mchezo huo.

Simba itamenyana na RS Berkane ya Morocco katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 13.

Ally amesema:”Taarifa ya awali kuhusu majeruhi ni kuwa Hassan Dilunga atakosekana kwenye mchezo wetu ujao.

“Taddeo Lwanga,Kibu Dennis, Chris Mugalu na Jonas Mkude wapo tayari kwa mchezo. Berkane wamekuja wakati mbaya maana wametukuta tuko kamili,”.

Tayari tiketi za mchezo huo zimeanzwa kuuzwa na kiingilio kwa mzunguko ni 3,000, VIP B & C ni 20,000 huku VIP A ikiwa ni 30,000.