KINARA wa utupiaji wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga, Fiston Mayele ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 100 awapo uwanjani kwenye kutupia pamoja na kutengeneza nafasi za mabao.
Ndani ya Ligi Kuu Bara ameyeyusha dakika 1,301 akiwa amefunga mabao 10 na ni mabao matano ametupia Uwanja wa Mkapa huku mabao matano ametupia nje ya Uwanja wa Mkapa.
Bao lake la kwanza alifunga Uwanja wa Majimaji, Songea mbele ya KMC na bao la 10 alifunga mbele ya Geita Gold Uwanja wa CCM Kirumba.
Ana hatari kila baada ya dakika 100 kwa kuwa amehusika katika mabao 13 ya Yanga akiwa ametoa pasi 3 za mabao.