YANGA NDANI YA DAR

KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo Machi 7 kimewasili salama Dar baada ya kuanza safari mapema leo wakitokea Mwanza.

Jana Machi 6,2022 Yanga ilikuwa kwenye msako wa pointi tatu na ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Bao la ushindi lilipachikwa dakika ya kwanza na Fiston Mayele ambaye anafikisha bao la 10 akiwa sawa na Relliats Lusajo anayekipiga ndani ya Namungo FC ya Lindi.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 45 baada ya kucheza mechi 17 na haijapoteza mchezo hata mmoja.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo ndani ya Yanga na walianza jana kikosi cha kwanza ni pamoja na Paul Godfrey na Sure Boy.