SIMBA YASEPA NA POINTI MBELE YA DODOMA JIJI

UWANJA wa Mkapa Simba leo Machi 7 imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliokuwa na ushindani mkubwa.

Ni mabao ya Clatous Chama dakika ya 55 kwa mkwaju wa penalti na Meddie Kagere ambaye alipachika bao hilo kwa kichwa akiwa ndani ya 18 ilikuwa dakika ya 74.

Kagere anafikisha bao la sita ndani ya ligi kwa msimu wa 2021/22 akiwa ni mtupiaji namba moja kwa kikosi cha Simba.

John Bocco nahodha alikwama kukamilisha dakika 90 kwa kuwa alipata maumivu nafasi yake ikachukuliwa na Kagere.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 37 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 17 huku vinara wakiwa ni Yanga wenye pointi 45 kibindoni.