KAPOMBE KUIKOSA DODOMA JIJI KWA MKAPA

BEKI bora katika kazi ngumu na chafu uwanjani Shomari Kapombe leo Machi 7,2022 anatarajiwa kuukosa mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji.

Kapombe aliumia katika mchezo uliopita mbele ya Biashara United na alikwama kuyeyusha dk 90 badala yake alitumia dk 30.

Aliweza kutoa pasi mbili za mabao yaliyofungwa na Pape Sakho pamoja na Mzamiru Yassin.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco amesema kuwa leo Kapombe hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoanza dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku, Uwanja wa Mkapa.