YANGA YAITUNGUA GEITA GOLD

Heritier Makambo, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa mchezo wao wa leo dhidi ya Geita Gold ulikuwa ni muhimu kwao kupata pointi tatu muhimu.

Baada ya dakika 90, ubao wa Uwanna wa CCM Kirumba umesoma Geita Gold 0-1 Yanga.

Bao pekee la ushindi limefungwa na Fiston Mayele ilikuwa dakika ya kwanza na liliweza kudumu mpaka dakika ya 90.

Mayele anafikisha mabao 10 na pasi 3 za mabao sawa na Relliants Lusajo wa Namungo mwenye mabao 10.

Kibindoni Yanga inafikisha pointi 45 ikiwa ni namba moja na bado haijapoteza.