NYOTA watano wa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo wanatarajiwa kuukosa mchezo wa ligi dhidi ya Geita Gold.
Ni Jesus Moloko, Djuma Shaban pamoja na Khalid Aucho ambao hawa hawapo fiti kuweza kuanza mchezo wa leo.
Aucho inaripotiwa kwamba amepata majeraha huku Djuma akitajwa kuwa na Mlaria na Moloko yeye ni majeruhi na alifanyiwa upasuaji hivi karibuni.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote zinasaka pointi tatu.
Pia yupo Yacouba Songne ambaye huyu ameanza program maalumu pamoja na Abdalah Sahibu, ‘Ninja’ beki ambaye ametumia dakika 2 uwanjani ilikuwa mbele ya Kagera Sugar kutokana na kutokuwa fiti.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na wanahitaji pointi tatu licha ya baadhi ya wachezaji kukosekana kutokana na sababu mbalimbali.
“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini tupo tayari ili kuweza kupata matokeo, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi tunaamini kwamba tutashinda,”.