NTIBANZOKIZA APEWA TUZO YA MCHEZAJI BORA

SAID Ntibanzokiza, Kiungo wa Yanga ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania imeeleza kuwa nyota huyo amechaguliwa na Kikao cha Kamati kilichokutana Dar Jumamosi.

Kwenye mechi za ligi aliweza kutupia mabao mawili na kuhusika katika mabao matatu.

Leo Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Geita Gold, Uwanja wa CCM Kirumba.