Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameteuliwa kuwa kocha bora wa Februari ndani ya Ligi Kuu Bara.
Kwa mujibu wa Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) iliyokutana Jumamosi ilimchagua Nabi.
Nabi ametwaa tuzo hiyo akiwashinda Fred Minziro wa Geita Gold na Thiery Hitimana wa KMC.
Kwa Februari Yanga iliifunga Kagera Sugar mabao 3-0, Mtibwa Sugar 0-2 Yanga na sare ya bila kufungana dhidi ya Mbeya City.
Leo Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Geita Gold, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.