UWANJA wa CCM Kirumba, ubao unasoma Geita Gold 0-1 Yanga ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Kasi ilianza kipindi cha kwanza ambapo Yanga walifanya majaribio mawili ambayo yalikuwa na hatari lakini ni moja liliweza kuzama nyavuni.
Ni Fiston Mayele alipachika bao hilo mapema dakika ya kwanza kutokana na safu ya ulinzi ya Geita Gold kushindwa kuwa na utulivu.
Linakuwa ni bao la 10 kwa Mayele ambaye ni mshambuliaji namba moja wa Yanga anakuwa sawa na Lusajo Mwaikenda ambaye anakipiga Namungo FC.