KLABU ya DTB inayoshiriki Championship leo Machi 5 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu FC ya Mbeya.
Ilikuwa ni mchezo mmoja wa kukata na shaka uliowakutanisha vigogo hawa wanaopewa nafasi kubwa ya kuweza kushiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.
Bao pekee la ushindi lilifungwa na Ally Ally wa Ihefu ambaye ni beki katika harakati za kuokoa na kufanya Ihefu wasiwe na chaguo.
Sasa DTB inafikisha pointi 49 huku Ihefu ikibaki na pointi zake 44 zote zikiwa zimecheza mechi 20.
Ikumbukwe kwamba mchezo wa leo ulikuwa mubashara @globaltvonline