UWANJA wa Mkapa ubao umesoma Simba 3-0 Biashara United na kuwafanya Simba kuondoka na alama tatu mazima.
Mabao yote yalipachikwa kipindi cha kwanza kwa upande wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Pablo Franco.
Ni Pape Sakho alipachika bao dk ya 8 ,Mzamiru Yassin di 13 na Clatous Chama di ya 17.
Majaribio ta Biashara United kupitia kwa Deogratius Mafie pamoja na Cristian Zigah hayakuzaa matunda na mapigo ya mipira iliyokufa ilikuwa kwa Ramadhan Chombo kwa upande wa Biashara United.
Medie Kagere alikosa penalti dk 90 baada ya James Setuba kuokoa penalti hiyo iliyosababishwa na Bernard Morrison.