MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Namungo, Relliats Lusajo ni baba lao kwa utupiaji ndani ya Bongo katika Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22.
Leo Machi Mosi anaanza mwezi mpya huku akiwa ni namba moja kwa kuwa ametupia mabao 10 akiwa na jezi ya Namungo FC.
Kwa mujibu wa rekodi za Bodi ya Ligi Tanzania,(TPLB) nyota huyo amecheza mechi zote 16 ambazo timu hiyo imecheza.
Ametumia jumla ya dakika 1,172 uwanjani na kuweza kufunga mabao hayo 10 na yote alifunga mzunguko wa kwanza.
Anayefuatia ni Fiston Mayele huyu anakipiga Yanga akiwa ametupia mabao 9 na pasi mbili za mabao.