JOHN Matambala, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa wana presha kubwa kwenye ligi pamoja na mechi ambazo wanazicheza kwenye Ligi Kuu Bara.
Leo Machi Mosi,2022 Azam FC itawakaribisha Coastal Union kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ubao ulisoma Coastal Union 1-1 Azam FC na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.
Matambala amesema:-“Tuko na presha kubwa kwa sasa hivi kwamba nyuma yetu kuna watu ambao tumelingana nao pointi lakini pia tupo na presha kwa ajili ya mechi yetu ili kuweza kupata matokeo mazuri.
“Tumejiaandaa kwa ajili ya kupata pointi tatu na wiki yote tulikuwa tunajiandaa ili kupata matokeo kwenye mchezo wetu dhidi ya Coastal Union.
“Coastal Union ni timu nzuri, timu bora na sisi tunawaheshimu wametoka kupoteza kwenye mechi zao ambazo wamezicheza lakini tupo tayari kwa ajili ya kupata pointi tatu muhimu na tunawaheshimu,”.