>

AZAM FC WATAMBIA REKODI ZA NYUMBANI,KESHO KUKIWASHA

ZAKARIA Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya Coastal Union hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.

Kwenye msimamo ikiwa nafasi ya 3 na pointi 24 itamenyana na Coastal Union iliyo nafasi ya 11 na pointi 17 zote zimecheza mechi 15.

Thabit amesema:”Mashabiki waje mapema utaratibu wa tiketi umefanyiwa kazi na tayari umefanyiwa kazi kwa kuwa awali ulikuwa unasumbua na hautajirudia tena, kesho pira Irizar litapigwa mashabiki waje kwa wingi tutacheza pira ice cream na tupo tayari.

“Tukuwa nyumbani huwa tunafanya vizuri na ni Agosti 20,2011 tulianza kuutumia Uwanja wa Azam Complex katika mechi za ligi kuu hivyo tunakwenda msimu wa 10.

“Mechi za ligi tumepoteza mechi tano tu hivyo tunapokuwa nyumbani huwa tunakuwa vizuri hasa nyumbani mashabiki waje.

“Wachezaji wametuahidi kwamba watatupa ushindi na tunawaheshimu Coastal Union lakini waje mashabiki wasiwe na mashaka,” amesema.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku kwenye msako wa pointi tatu muhimu.