AHMAD Ally, Kocha Msaidizi wa KMC amesema kuwa wanazitaka pointi tatu mbele ya Polisi Tanzania.
Ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza mechi 15 ipo nafasi ya 8 leo inakutana na Polisi Tanzania, Uwanja wa Azam Complex.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ally amesema kuwa mbinu zote zitajulikana leo watakapokuwa uwanjani.
“Hatuwezi kuweka wazi mbinu tutakazotumia kuwakabili wapinzani wetu kwa kuwa tunajua ni timu nzuri na imara hivyo tutabainisha mbinu zetu kwa vitendo.
“Utakuwa mchezo mgumu na kila timu inahitaji ushindi hivyo kikubwa ni kwa mashabiki kuweza kujitokeza kuona namna gani tutaweza kutoa burudani,” amesema.
Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliowakutanisha wababe hawa ni Polisi Tanzania ilishinda kwa mabao 2-0 na mtupiaji alikuwa ni Vitalis Mayanga.