KMC WALIPA KISASI MBELE YA POLISI TANZANIA

KMC leo imelipa kisasi mbele ya Polisi Tanzania kwa kuwatungua mabao 3-0 na kusepa na pointi tatu mazima.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Karatu, ubao ulisoma Polisi Tanzania 2-0 KMC na kuwafanya waweze kusepa na pointi tatu mazima.

Katika mchezo wa leo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, ubao umesoma KMC 2-0 Polisi Tanzania.

Mabao yalijazwa kimiani na Idd Kipagwile dk 15, Emmanuel Mvuyekule dk 73 na Sadalla Lipangile dk 88.

Ushindi huo unaifanya KMC kufikisha pointi 22 ikiwa nafasi ya 6 na Polisi Tanzania inabaki na pointi 19 ikiwa nafasi ya 9 katika msimamo.