FEISAL Salum, kiungo mwenye uwezo wa kutumia miguu yote miwili kufunga pamoja na mikono amekutana na jambo litakalomfanya kesho aukose mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar.
Nyota huyo anakumbukwa kwamba alikuwa ni nyota wa kwanza ndani ya Yanga kwa msimu wa 2021/22 kufunga bao la mkono mbele ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu na alionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi wa kati
Pia ni mchezaji wa kwanza msimu huu ndani ya Yanga kuweza kufunga bao kati ya 25 ambayo yamefungwa na timu hiyo inayoongoza ligi.
Kadi hiyo ya njano ambayo alionyeshwa kutokana na kufunga bao la mkono inamfanya aweze kuukosa mchezo wa kesho dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi cha kesho ambacho kitamenyana na Kagera Sugar.
“Feisal Salum kesho hatakuwa sehemu ya kikosi dhidi ya Kagera Sugar kwa sababu ana adhabu ya kadi ya njano hivyo hatacheza, lakini Yassin Mustapha yupo fresh,” amesema.
Kwenye mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Kaitaba Yanga ilishinda bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Feisal.