HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kwamba ushindi ambao wameupata mbele ya Mtibwa Sugar ni muhimu kwao na wameweza kupata ushindi huo mbele ya Uwanja wa Manungu ambao unatajwa kuwa ni machinjio ya Mtibwa.
Yanga ilifunga mzunguko wa kwanza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na mabao yalifungwa na Said Ntibanzokiza pamoja na Fiston Mayele.